Tulonge

DIAMOND AFUNGUKA NA KUONGELEA MPENZI WAKE MPYA...!!!

Mwimbaji Diamond Platnumz amekiri kwamba kwa sasa ana mpenzi mpya ambae sio maarufu kabisa.
Ameamplfy jana kwamba “tuna kama mwezi hivi toka tumeanza kuwa pamoja, sio vizuri sana kumzungumzia kwa sababu naogopa sana drama mwisho yasije yakawa yale yale tena ndio maana nafanya siri lakini sio maarufu na wala sio Jokate.”

Mtangazaji wa Amplifya Millard Ayo alipomuuliza kama ataingia tena kwenye mapenzi na mtu maarufu ambako ndiko alikotoka, Diamond amesema “kwa kweli siwezi kujua kwa sababu kila kitu kinaandikwa na mapenzi ni kama ajali.”

Diamond aliwahi kukanusha exclusive on millardayo.com kwamba hana uhusiano wa kimapenzi na mrembo Jokate ambae walianza kuzungumziwa sana baada ya Jokate kushuka kwenye gari moja na Diamond wakati wakiwasili kwenye show ya Mlimani City wiki kadhaa zilizopita.

Kwenye hiyo benz alishuka Diamond na mama yake mzazi pamoja na Jokate na Diamond alipoulizwa na millardayo.com alisema siku hiyo alitakiwa kushuka na mamodo wawili lakini mmoja ambae ni Lisa alishindwa kuja siku hiyo kwa hiyo ikabidi ashuke na Jokate tu.

Source: Millardayo.com

Views: 1104

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Bonielly on April 24, 2012 at 12:08

huyu dogo swaga zimezidi mwisho wa siku atatulia siku haijafika,

Comment by ANGELA JULIUS on April 23, 2012 at 16:24

YOTE KHERIIIIII

Comment by Holiness Bangereza on April 22, 2012 at 16:23
Ye anasema Wema ndo anapenda kulipa waandish ili atoke kwa magazeti. Afu ameulizwa kama atadate tena star akajibu sijui mana Mungu ndo anapanga.

Yan mi mwanaume ambae hana uhakika na mahusiano yetu kwakwel simtak.

Ngekua ndo huyo dem mpya wa Diamond afu nkaona statment kama hyo kwakwel cjui ingekuaje.
Comment by ILYA on April 21, 2012 at 11:47

Hapana wadau,!!!

NAOMBA MNISOME KAMA IFUATAVYO:

unajua kwa mujibu wa mtazmo wangu kila mtu ana jinsi ya kutoka,wakati wengine wanajiuliza nitoke vipi kuna wengine upande wa pili wameisha ona jinsi ya kutoka.unajua ukisubiria mtu akutoe uwe maarufu na kukufikisha unakotaka kufika wewe binafsi utachelewa sana ndugu yangu kufika kule ndoto zako ziliko elekea,lakini ukiwa na mbinu za kujitoa mwenyewe basi utakuwa maarufu kwa muda mchache sana na katika umri mdogo.

Mr diamond,ni mbunifu sana wa njia mubadala na barabara za kujitoe yeye kama yeye,moja ya njia zake hizo ni kujitangaza katika media,iwe kwa kuwalipa watangazaji au kivyovyote vile,muhimu kunyanyua utajo wake kwa mashabiki na watanzania kwa ujumla na ikiwezekana nje ya Tanzania.

Tusiangalie yeye kuwalipa hao watangazaji tuangalie natija na malengo yake.Na istoshe sio vizuri kula peke yako kuna wakati mwingine utoe rizki kwa wengine nao wafaidike na wewe,kitendo cha yeye kuwalipa watangazaji ili watangaze habari zake kwa media na magazeti inayonyesha ni jinsi gani kijana huyu alivyokuwa tayari kula wenzie,anavyojua jinsi gani ya kuitengeneza njia za wenzie nao kujipatia kipato na rizki,na mtu huyo anayejali wenzie kwanini wenzie nao wasimjali na kumtangaza na kukuza jina lake.!!!!

Watu ndivyo namna hiyo wanavyoendesha mambo yao na kukuza kwa speed ya ajabu majina yao,lakini mkono wako ukiwa wa birika hutaki hela yako itoke,basi hata umaarufu wako utachechemea na pengine wakati mwingine huenda hata watu wakakusahau kama upo katika fani.

Maisha kutegemea na kupeana,usitake kila wakati ufunge wewe goli tu,tengeneza pass na wengine wafunge,tuma cross na wengine waunganishe kwenye goli wote mfurahi,lakini ukitaka kufunga wewe kila wakati,basi ujue wachezaji wengine nao wataacha kukutengenezea pass na hawatakutumia cross ili uunganishe kwenye nyavu,unapokuwa uwanjani jitahidi kushirikiana na wachezaji wenzako,maana huwezi kuwa Lionel Messi wa Barcelona kama hujashirikiana Xavi Hernandez au huwezi kuwa Robin van Persie  wa Arsenal kama hujashirikiana uwanjani na Bacary Sagnia.

NA HUO NDIO MTAZAMO WANGU KUHUSU DIAMOND,KWA MAANA KWAMBA:

HAWEZI KUWA STAR MAARUFU TANZANIA NA NJE YAKE KAMA HASHIRIKIANA KWA KARIBU NA WATANGAZAJI NA WATU WA MAGAZETI WENYE KUCHUKUA SEHEMU KUBWA YA KUTANGAZA UMAARUFU WA MTU AU SEHEMU KUBWA YA KUKUZA UMAARUFU WA MTU.

Comment by Dixon Kaishozi on April 20, 2012 at 16:13

Anatafuta umaarufu kwa "nguvu"..

Comment by cecilia kayombo on April 20, 2012 at 13:26

mmh Dis lbd yy ndo anawapa hela waandishi ili wamuandike..lol

Comment by Tulonge on April 20, 2012 at 9:50

Nahic huwa wanampa hela ili waandike habari zake, mbona habari za wasinii wengine haziandikwi hovyo hovyo.Kuna kina AY,Mwana FA,Professor J nk huwa hawaandikwi kivilee kama huyu.

Comment by Christer on April 20, 2012 at 7:37

Anataka uza magazeti @ Dis.

 

Comment by Tulonge on April 19, 2012 at 23:59

Huyu dogo kazi ya kuweka mambo yake hadharani ndomaana anapata matatizo.Sijui kwa nini hajifunzi?

© 2016   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* /*