Tulonge

Viumbe wasioonekana wazidi kuichafua Dunia!

Sayari yetu hii ya dunia baada ya kuumbwa ilikaa miaka mingi mno kabla ya kukaliwa na viumbe wanaoitwa Binadamu.Ambao hapo zamani walitanguliwa na viumbe wengine wajulikanao kama Majini.

Majini ni viumbe walioumbwa kwa moto,miili yao ni miepesi inayowezakupenya sehemu yoyote,tena mwanadamu hana uwezo wa kuiona miili hiyo kwa macho.

Wanao uwezo wa kusafiri masafa marefu kwa muda mfupi,unaoweza kuishangaza akili ya mwanadamu.Kana kwamba wanatumia kasi ya mwanga {nuru},yaani kilometa 300,000 kwa sekunde moja !.

Majini ni viumbe tunaoishi nao duniani,lakini hupenda kujitenga mbali na makazi ya watu,ndio maana huishi misituni,baharini pamoja na majangwani.

Majini hukaa kwa matabaka {koo} na wapo tayari kumshambulia mtu yoyote atakayetaka kuyaharibu makazi yao,na kama yatashindwa vita,basi yatalihama eneo hilo na kwenda kuishi katika eneo lingine.

Mashetani pia ni katika matabaka ya majini,ingawa wao huogopewa sana kutokana na uhusiano wao wa karibu na Ibilisi ambaye ni Baba yao na ndiye huyu anayetusumbua kila siku kwa vishawishi vyake pamoja na kututia wasiwasi ndani ya mioyo yetu.Historia inaonyesha kuwa mashetani ndio waasisi wa uchawi.

Baada ya kifo cha Nabii Suleiman Mwana wa Daud {a.s},mashetani walidai kuwa Nabii Suleiman alikuwa akiwatawala watu kwa kutumia njia za kichawi ndio maana aliwezakuwatawala majini na watu.

Walipata wafuasi wengi mno waliojitokeza kwenda kujifunza uchawi kwa malengo ya kuwadhuru wengine pamoja na kuwatawala.

Rejea Surat Albaqarat Aya 102-103.Ingawa Mwenyeezi Mungu aliwakataza watu kutofuata uzushi wa mashetani dhidi ya Suleiman {a.s} ila watu hawakujali wala kusikia baada ya kunogewa na mafunzo ya kichawi.

Wakaendelea na mafunzo hayo ya uchawi ambayo kwao hayakuwa na faida bali hasara siku hiyo ya malipo.

Cha ajabu ni kwamba inasemekana kuwa hata baadhi ya wasomi na wavumbuzi wa vitu duniani wana uhusiano na mashetani katika kuwasaidia kubuni na kuvumbua vitu vya kisasa,vinavyoweza kumvutia mwanadamu viingiapo Sokoni.

Vitu hivyo ni kama vile: Magari ya bei kubwa,TV,na hata simu za mkononi.Watu hao wenye mahusiano na mashetani hujulikana kama FREEMASONS,na kwa bahati mbaya ndio wanaozidi kulishika soko la dunia kibiashara,wanaenea kwa kasi kote duniani huku wakifanya ufisadi na uharibifu baada ya kuwarubuni watu kwa kuwaahidi utajiri mkubwa iwapo watu hao watakubali kufuata dini ya Shetani !.

Na Chalii_a.k.a_ILYA

Views: 4325

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Tulonge on June 7, 2012 at 7:57

Kwa jina la Yesu hiyo midude huwa inakimbia.

Comment by ILYA on June 6, 2012 at 21:16

Shem habari ndio hiyo@,uchunguzi wa kina unaonyesha hao wataalamu wa ugunduzi wa vitu vya kileo,hisaidiwa sana na mashetani katika kuwasaidia kuvumbua vitu kama hivyo,huwapa siri na mbinu mbali mbali za kitaalamu ili waweze kuvumbua vitu ambavyo vikiingia sokoni basi watu vinabamba,utaona watu wakipishana sokoni ili kununua bidhaa hizo mpya.

Comment by ANGELA JULIUS on June 6, 2012 at 18:07

shemeji wewe mkareeee, ulichosema hapo kwenye hiyo habari ni kweli kabisa Mungu atunusuru Amein

© 2016   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* /*