Tulonge

Nyumba za NHC Kibada kuanza kuuzwa wiki hii; Bei haitazidi Mil. 50/=

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) litaanza kuziuza nyumba zake zinazojegwa katika eneo la Kibada katikati ya wiki hii.

NHC iemesema nyumba zake 216 zinazojengwa katika maeneo hayo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam, hazitauzwa kwa zaidi ya Shilingi milioni 50, ili kumwezesha mwananchi wa kawaida kuzinunu.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mikoa na Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea miradi ya ujenzi wa nyumba za shirika hilo.

“Kigamboni pale Kibada tuna nyumba za aina mbili, yaani zipo za vyumba viwili na nyingine za vyumba vitatu. Kwa kuwa lengo letu siyo kupata faida bali ni kuwasaidia wananchi ili waweze kumiliki nyumba badala ya kuendelea kupanga, nyumba hizo zitakapoanza kuuzwa hazitauzwa kwa zaidi ya Sh milioni 50.

Pamoja na kwamba lengo letu ni hilo, bado tunaiomba Serikali iondoe VAT kwa vifaa vya ujenzi ili nyumba ziweze kuuzwa kwa bei ya chini zaidi,” alisema Mndolwa.

Naye, mmiliki wa Kampuni ya Shibat Enterprises Limited, Edwin Shitindi ambayo imepewa tenda ya kujenga nyumba 104 katika eneo hilo la Kigamboni, alisema atahakikisha nyumba hizo zinakamilika ndani ya miezi mitano kuanzia sasa. Alisema kampuni yake itajitahidi kuzijenga katika ubora unaotakiwa kwa kuwa zitakapoanza kutumika zitatumiwa na Watanzania.

Wadau ambao wana nia ya kumiliki nyumba kwenye eneo hilo wanashauriwa kutembelea tovuti ya NHC (www.nhctz.com) kuanzia Jumatano ya wiki hii ili kupata maelezo zaidi juu ya bei, ulipaji na umiliki wa nyumba hizo.

Chanzo: wavuti.com

Views: 1104

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by Mama Malaika on December 20, 2012 at 23:27

Ni kweli ujenzi wa nyumba unasumbua sana ila kwa upande wangu ni bora nijenge mwenyewe inanipunguzia gharama kwani nina-design mwenyewe na kuchora ramani mwenyewe. Nimesimamia nyumba zangu kuanzia foundation najua imeingia nondo ngapi za unene gani, na kuta muhimu ambazo zina support building structure nazitazama zinavyojengwa huku engineer mkuu ni mume wangu, mafundi tunakaa nao hadi jioni hatubanduki. Likizo yetu ikiisha ujenzi unasimama hadi tutapokuwa likizo tena ndio ujenzi unaendelea, siamini kuachia ndugu wala nani.

Comment by Mama Malaika on December 20, 2012 at 22:53

Hizi nyumba ni kweli wanauziwa wananchi au wanazuga tu na kuuziana wao kwa wao vigogo na familia zao halafu wanakuja zipangisha kama walivyofanya zile za NHC kule Mbweni JKT? Kwa ujenzi ule nilioona Mbweni wanavyojenga foundation, wala siwezi nunua bora nikanunue nyumba za NHC za zamani halafu nikarabati mwenyewe kwani zilijengwa kwa uhakika.  

Comment by Alfan Mlali on December 20, 2012 at 12:58

Tena unaweza kuta fundi anakujengea nyumba huku na yeye anajenga ya kwake kwa hela hizo hizo unazotoa wewe.

Comment by Tulonge on December 19, 2012 at 21:09

Halafu baadhi ya mafundi wezi kweli, inabidi kila siku uwesimamie.Huo muda unatoka wapi

Comment by Alfan Mlali on December 19, 2012 at 12:15

Kweli kabisa Dismas. Mimi kwa kweli iko siku nikizikamata nanunua tu.Issue ya kuanza kuumiza kichwa kuhusu kiwanja, matofali,mchanga,kokoto,mbao,mabati,wizi wa mafundi.nk siwezi kwa kweli.

Comment by Tulonge on December 19, 2012 at 0:23

-Binafsi huwa naona ni bora kununua kuliko kujenga.Mziki wa kujenga ni balaa, lazima ujipange.Wenye hela mkononi bora mnunue.

-Halafu hapa ni kwa uhakika zaidi, kuliko zile ishu za kuuziana viwanja kienyeji halfau unajenga nyumba hadi mwisho.Baadae serikali inakuja kusema hiki kiwanja hukuuziwa kihalali.

© 2016   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* /*