Tulonge

Kahama: Binti achinjwa kinyama na mpenzi wake

Jessica Elialinga baada ya kuchinjwa.

VILIO vilitawala Kata ya Nyahanga wilayani hapa wakati wa kuuaga mwili wa binti Jessica Elialinga (19) aliyeuawa kinyama kwa kuchinjwa kama kuku na mpenzi wake, Musa Petro (27) mkazi wa Shunu kwa sababu zinazodaiwa ni wivu wa kimapenzi.
Tukio hilo lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana, lilijiri saa 12:45 Februari 6, mwaka huu.

 

Kitendo hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la kutaka kujitoa roho kwa kisu.

 

Akisimulia juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.

Muuaji Musa Petro.


“Unajua Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake kama mzaha.

 

“Alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kwa mpenzi wake huyo tangu walipoanza uhusiano, msichana akiwa kidato cha pili, lakini anatoka kimapenzi na mwanaume mwingine,” alisema rafiki huyo.

 

Hata hivyo, inadaiwa baada ya mtafaruku wa usaliti, wawili hao walipatana na kuendelea na mapenzi, lakini baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha nne alibadilika ambapo mwanaume alisikia kuwa tayari ana mwanaume mwingine kutoka jijini Mwanza ambaye walikubaliana kufunga pingu za maisha baada ya kumaliza masomo.

Jessica Elialinga enzi za uhai wake.


Inadaiwa siku chache kabla ya mauaji hayo, rafiki mmoja wa karibu wa mtuhumiwa alikutana na marehemu njiani na kumsimamisha kwa lengo la kumweleza kauli zenye kutishia maisha yake anazozitoa mpenzi wake, lakini binti huyo hakusimama kumsikiliza.

Baada ya Musa kudaiwa kufaulu kumchinja mpenzi wake huyo na yeye kujikata koromeo na kuanguka akiwa ameishiwa nguvu, kijana mchunga mbuzi ambaye wengi katika eneo hilo humchukulia kama kaka yake Jessica, ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshuhudia Musa akiwa katika hali hiyo.

Alipomhoji kulikoni, hakupata jibu zaidi ya kushuhudia jitihada za mtuhumiwa huyo kufungua mlango wa chumbani mwake zikishindikana.

Kijana huyo alitoa taarifa kwa watu ambao walifika na kumchukua Musa na kumkimbiza hospitali ya wilaya kuokoa uhai wake.

Watu waliobaki nyumbani walifuatilia michirizi ya damu hadi kwenye zizi la mbuzi ambako walimkuta Jessica ameshafariki dunia baada ya kuchinjwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Everest Mangala alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kahama katika Hospitali ya wilaya hiyo anakoendelea kupatiwa matibabu.

Via: audifacejackson.blogspot.com

Views: 582

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ILYA on March 20, 2013 at 21:12

Kweli mama mkwe,ukimkosa unayempenda haina maana warembo wameisha bwana,mbona wapo kibao wazuri tu,ni vibaya sana kuendeka hasira kuliko kujimiliki,maana kweli matokeo ya hasira huwa ni hasara.

Comment by Mama Malaika on March 20, 2013 at 16:00

Mapenzi hayaui bali binadamu ndio wanaua (wauaji)!! Ukisikia hasira hasara ndio huyu bwana, iwapo kijana aliona msichana wake anaenda pembeni basi ilipasa akubali yaliyotokea ingawa roho inauma baada ya muda yangepita na siajabu angepata binti mwingine mrembo zaidi.

Comment by Christer on March 19, 2013 at 8:33

Mapenzi ni matamu sana mnapoelewana na kusikilizana na machungu mnapotofautiana hasa kusalitiana n.k ila mmmh ukiona yamekushinda jua hayakua yako hayo, yako yapo kwa mtu mwngne, achaneni kwa amani km mlivyoanzana na i love u nyiiiingi, i miss u za kutosha! RIP Binti, gone soon!

Comment by Omary on March 15, 2013 at 21:18

Nikweli mapenzi yanauwa ila MUNGU nisaidie nisimuuwe mtu kwaajili ya mapenzi pia kumegewa kisela kunauma ila ukigunduwa unamegewa kama kweli unauhakika umethibitisha hasaa kuwa mchizi anamega kisela bora umsepeshe shory wako kwa amani kabisa maana atakuletea magonjwa na mambo mengine kama haya ya kuuwana maana kama hujamuuwa kwa hasira atakuuwa wewe kwa magonjwa vyote vifo ila hiki ni cha kinyama umchinje mtu kama kuku? tena mko wawili tu? dah! jamaa ni hatari sana huyu mimi naogopa hata kumchinja kuku namuonea huruma huyu mchizi kamchinja mtu tena mrembo wake dah! yaani hajamfikiria hata yale mazuri waliopeana maana katika maisha kuna mazuri na mabaya so mwenzio akikuudhi rudisha mkanda nyuma kuna aliokufurahisha na umsamehe kaeni ongeeni ikishindika gawaneni njia kila mtu arudi kwa Mamaake na watoto waende kwa Mamaao

Comment by ILYA on March 15, 2013 at 16:11

Pole binti najua ulikuw abado unahtaji kuishi hadi mwisho wa uhai wako uliopangiwa na Mola!.Inauma sana,mapenzi yanahitaji control,kusikilizana na kuelewana,lakini kikubw azaidi katika mapenzi ni kuaminiana na sio kila wakati kutuhumiana kwamba wewe unanisaliti,na vitu kama hivyo maana tuhuma kama hizo katika mapenzi hupanda kitu kibaya sana katika fikra za wapendanao na matokeo yake kuzaa shari kama hii inayoonekana ktk news hii. 

© 2016   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* /*