Tulonge

Nyerere alishikwa hasira zaidi juu ya telegram aliyotumiwa na nduli Iddi Amini

Katika barua hiyo Dada alimmwambia mchonga hivi : "Nataka nikuhakikishie kwamba nakupenda saana, na  kama ungelikua mwanamke basi ningefikiria jinsi ya kukuoa japo kichwa chako kimejaa mvi. Lakini kwakuwa wewe ni mwanaume basi uwezekano huo haupo"............. Kwa Kashfa hii Nyerere hakujibu kitu maana alijua siku ya huyu mshenzi inakaribia.

Views: 1233

Add a Comment

You need to be a member of Tulonge to add comments!

Join Tulonge

Comment by ILYA on November 18, 2011 at 22:33

Hahaha mama Mkwe umenifurahisha sana,umenimegea kahistoria katamu sana.Mama mkwe inaonekana computer yako iko makini kw akuhifadhi haina virus,sijui unatumia Antivirus NOD32,! maana umenipa matukio yanayokwenda sambamba na hadithi alizokuwa akinihadithia babu yangu kuhusu Amini Dada.

Asante sana kw ahistoria mkwe,amini kweli alikuwa fyatuka akili,sasa chupi hiyo alikuwa anataka ya nini?! avae au?au alitaka kuininginiza scan kwake ionekana kama tuzo,hahahahah,Enewei,Mwalimu Nyerere alikosea sana ilitandika amtandike masikio kwa kutumia kile kifimbo chake.

Na nadhani huko walipo kwa sasa watakuwa wanakumbushana mitikasi yao iliyojiri baina yao duniani.

Comment by Mama Malaika on November 18, 2011 at 22:30

Kunambi, Angela & Dismas karibuni kwani hii ndio raha ya social networks, tunapeana habari kama nanyi mnavyonipa habari za kizazi cha Bongo Flava nisizozijua. Ha haa haaa

 

Kunambi... mie napenda Dismas atuwekee kipengelee cha hadithi za makabila tofauti ya Tanzania. Ha haa haaa 

 

Dismas.... Idi Amin alikuwa ana plan mambo yake anavyojua yeye na wakati mwingine alipanga kutokana na ndoto zake anazoota usiku. Alikuwa m-babe sana yule jamaa (Mungu amrehemu). Alijisifia kuwa kasomea mafunzo ya juu ya kijeshi kwenye Chuo kikubwa cha kijeshi cha kifalme nchini Uingereza cha Sandhurst na kujipa cheo cha juu cha kijeshi cha u-Field Marshal kitu ambacho kimekanushwa na utawala wa chuo cha Sandhurst kuwa Idi Amin hajawahi soma kwenye chuo chao. 

Comment by Tulonge on November 18, 2011 at 19:28

Duh! Mama upo juu, kumbe hili jamaa lilikua zero kabisa. Sasa sijui lilikuwa lunaweza vp ku-plan mambo yake kama kichwa chake kilikuwa kimejaa matope kiasi hicho.

Comment by ANGELA JULIUS on November 18, 2011 at 16:35

MAMA MALAIKA NAKUFAGILIA DADA YANGU LOL NA KWELI KUNA MAMBO AMBAYO HATA MIMI BINAFSI NILIKUWA SIJAWAHI KUYAJUA KUHUSU HUYU NDULI LOL BE BLESSED KWA UFAFANUZI HUU NDO UFAFANUZI UNAOTAKIWA ASANTE KWA KUCHUKUA MUDA WAKO KUTUELEZEA ON THE STAGE.

Comment by KUNAMBI Jr on November 18, 2011 at 15:01

Daaaah mama malaika kweli umenambia mambo hata me sikuyafaham maana wakati huo nahisi  hata tumboni kwa mama hakujua kama atakuja kubeba kiumbe kitakachokuja kuitwa Kunambi teh teh teh ndo raha ya kukaa na mama mwenye busara kama wewe, sasa nitamwambia Dis aweke na kipengele kile cha Hadithi Hadithi...... hadithi njoo,utam kolea teh teh uwe unatupasha habari za zamani kidogo

Comment by Mama Malaika on November 18, 2011 at 14:01

Idi Amin alikuwa fyatu kweli kweli kumwambia Mwl Nyerere waingie ulingoni kupigana ngumi huku mkono wake mmoja Amin ataufunga kwa kamba nyuma mgongoni, ukifikiria umbo la Nyerere lilivyo dogo na Idi Amin ni kipande cha mtu nasikia alikuwa mrefu 6ft 4in.

Hotuba za Idi Amin daima zilikuwa vituko na wakati mwingine vichekesho kama vile story za makuli wabeba mizigo sokoni. Nafikiri pia "fame" itakuwa ilichangia kichwa chake kuwa hivyo. Hebu fikiria Idi Amin hakuwa na elimu, alipokuwa kijana/mtoto aliuza maandazi mtaani kabla ya kuwa mpishi wa barracks za jeshi la KAR (king's African Rifle) na baadae kubebwa kwa tabia ya utiifu kwa maboss wake hadi kufikia vyeo vya juu, fikiria mtu kama huyo kuongoza nchi atakuwaje kama sio kufyatuka akili? 

Kali zaidi ilikuwa ya kituko chake cha mwaka 1972, kama viongozi wengine wa Commonwealth countries, Idi Amin alialikwa na Queen Elizabeth II kuja kusheherekea Queen Elizabeth's Silver Jubilee. Basi Amin akamwambia Queen Elizabeth ampatie chupi yake iliyo na miaka 25 kama zawadi kwa Amin ya sherehe hiyo. Nasikia Queen alimchunia Amin hadi sherehe inakwisha na Amin kuondoka. Amin alivyokichaa akaomba kumuoa Princess Anne (binti wa Queen Elizabeth).  

Hata yule mama aliyekuwa waziri mkuu wa taifa la Israel (bibi Golda Meir) miaka ile nasikia Amin aliwahi mnataka kuwa mkewe. Na siajabu siku moja angemla nyama maana kichwa cha Amin hakikuwa sawa.

Comment by Bonielly on November 18, 2011 at 12:50

mbona hausemi mungu mbaliki bonielly ulivyokuwa na roho ya kwanini@angela,,,,,

Comment by Bonielly on November 18, 2011 at 12:46

hembu soma miaka yangu hapo kwenye profile yangu weye acha ngenga mtoto wa kisukuma weye,,,,,,, unaona wote watoto nini? wakati wa kufunga mikanda namimi nimefunga nitafute nikuonyeshe mvi, ndio uamini hivi unaona mimi ni saizi yako nini?

Comment by ANGELA JULIUS on November 18, 2011 at 12:37

JAMANI BONIELLY WACHA KUTUDANGANYA HAPA WEWE KIPINDI CHA IDDI AMINI ULIKUWA UMEZALIWA KWELI ? WAKATI WEWE NI WA JUZI TUU HAPO MIAKA YA 1990 LOL MWOGOPE MUNGU, MANAKE UMEONGEA KANA KWAMBA ULIKWEPO ILA UKINIAMBIA UMESOMA HISTORY HAPO NAWEZA KUKUELEWA AU UMEWASIKILIZA WAKUBWA WAKIMWAGA LECTURE KUHUSU HUYU MWANADADA HAPO NAWEZA KUKUELEWA MANAKE NA WEWE MASIKIO WALUUUU, LOL HA HA HA

 

BINAFSI NALISIFU JESHI LETU KUMTANDIKA HUYU NDULI. MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU IBARIKI AFRICA

Comment by Bonielly on November 18, 2011 at 10:58

nilichompendeaga idiamini kujichanganya, halinaga mpango wa kulindwalidwa, ila alinikeraga na matabia ya ukatiri, ushenzi ufirauni, kuropokaropoka hovyohovyo tu, sasa ile kuropoka ndio kilichomponza,

© 2016   Created by Tulonge.   Powered by

Badges  |  Report an Issue  |  Terms of Service

/* /*